Yatupasa
Kushukuru
Mtu mmoja
alistaajabu sana niliposema nitamshukuru Mungu
Baada ya
matatizo mengi kunipata akili yangu ikampa wasiwasi
Kwa kweli
nami, ilinigharimu, kujijulisha inipasavyo
Ila baada ya
muda nikaona yapo mengi ya kunifanya nimshukuru Mungu
Yako mengi,
hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu
mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
He ee jiunge nasi,
tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote
tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu
wetu
Ambassadors
of Christ tuashukuru lakini kwa wengi hatueleweki
kutokana na mambo
ya yaliotupata ili kushukuru si jambo la busara
Lakini ndugu,
ukitulia, nakujiuliza ya ajali ile
Tungeweza
kuangamia wote kwa pamoja asiwepo hata mmoja wa kusimulia
Majaribu
kama haya yalikuweko hata kwenye siku za mababu zetu
Ila kwa yote
walikuwepo mashujaa walioweza kuitetea imani yao
Tuwake Mungu, wakati wote, kwa yote hatujitegemei
Tukiwa hai
tukiwa mauti tuwake tujualo ni moja kushukuru
No comments:
Post a Comment